Tarehe ya Mwisho Kusasishwa: Septemba 26, 2014

SWYPE NA MKATABA WA LESENI YA MTUMIAJI WA MWISHO WA DRAGON DICTATION

HAYA NI MAKUBALIANO YA KISHERIA KATI YAKO (MTU BINAFSI AU KAMPUNI INAYOTUMIA SWYPE NA/AU DRAGON DICTATION APPLICATIONS) NA NUANCE COMMUNICATIONS, INC. ("NUANCE"). TAFADHALI SOMA MASHARTI YAFUATAO KWA UANGALIFU.

LAZIMA UKUBALI MASHARTI YA MAKUBALIANO HAYA YA LESENI YA MTUMIAJI ("MAKUBALIANO") ILI KUSAKINISHA NA KUTUMIA PROGRAMU YA SWYPE NA/AU HUDUMA ZA DRAGON DICTATION. KWA KUBOFYA KWENYE KITUFE CHA "KUBALI", UNAKUBALI KUZINGATIA MASHARTI YA MKATABA HUU. HUENDA USITUMIE PROGRAMU YA SWYPE AU HUDUMA YA DRAGON DICTATION KATIKA NJIA YOYOTE ISIPOKUWA UMEKUBALI SHERIA NA MASHARTI HAYA.

Programu ya Swype na Dragon Dictation inajumuisha programu fulani za mteja/seva zinazoruhusu watumiaji wa vifaa kudhibiti operesheni fulani za bidhaa kama hizo kupitia ingizo la maandishi na amri za matamshi, pamoja na, lakini bila kuegemea katika, uwezo wa kuunda ujumbe wa maandishi na barua pepe. Sheria na masharti yafuatayo yanakuruhusu kupakua, kusakinisha na kutumia programu ya Swype, pamoja na rogramu nyingine za ziada za Swype ambazo Nuance na wasambazaji wake wanaweza kukuletea, ("Programu"), inayotoa mfumo wa ingizo na kuruhusu watumiaji kufikia programu za seva za Dragon Dictation zilizosakinishwa katika kituo cha Nuance ("Huduma"), na pamoja na hati zilizotolewa na Nuance kwa kutumia Programu na kufikia Huduma.

1. IDHINI YA LESENI. Nuance na wasambazaji wake hukupa leseni ("Leseni") binafsi, isiyo ya kipekee, isiyohamishika, isiyogawanywa, isiyokataliwa, kwenye fomu ya kipengee tu, ili kusakinisha na kutumia Programu kwenye Kifaa kimoja. na kufikia Huduma kupitia Programu kwenye Kifaa kama hicho, katika nchi na lugha pekee katika Programu na Huduma zimefanywa kupatikana na Nuance na wasambazaji wake. "Kifaa"ni kifaa cha mkononi kilichoidhinishwa kama ilivyoelezwa kwenye tovuti ya Nuance, iliyo kwenye http://www.nuancemobilelife.com, inayoweza kusasishwa na Nuance mara kwa mara. Unathibitisha zaidi na kukubali kuwa Nuance inaweza kuunda vipakuliwa vya ziada vya Programu, pamoja na lakini bila kuegemea katika lugha, kibodi, au kamusi, na kuwa unaweza tu kutumia vipakuliwa kama hivyo vya ziada vya Programu na Programu iliyotolewa humo, na kwamba matumizi yako ya vipakuliwa kama hivyo vya ziada vya Programu vinazingatia sheria na masharti ya Mkataba huu. Unawajibika kwa ada zozote zitakazotokea na zinatozwa na mtu mwingine (kwa mfano, Google, Amazon, Apple), zinazoweza kubadilika mara kwa mara, kulingana na upakuaji wako na matumizi ya Programu na Huduma. Nuance haina jukumu la kurejesha malipo yoyote yaliyofanywa kwa wahusika wengine kama hao kwa matumizi yako ya Programu au Huduma kama ilivyowekwa kwenye Mkataba huu. Unathibitisha zaidi na kukubali kuwa Programu na Huduma zitatumia mtandao wako pasiwaya ili kutuma na kupokea data, na kwamba opareta wako wa simu na wahusika wengine wanaweza kukutoza mjazo wa Programu na Huduma, data na/au ada za matumizi.

2. MAJUKUMU YA LESENI.

2.1. VIKWAZO. Huwezi (isipokuwa kama ilivyoidhinishwa kisheria): (a) wasilisha maswali yoyote otomatiki au yaliyorekodiwa kwa Programu au Huduma isipokuwa vinginevyo iidhinishwe katika maandishi na Nuance; (b) tumia Programu na Huduma kando na matumizi yako binafsi; (c) fikia Huduma kwa programu au mbinu nyingine kando na Programu; (d) kunakili, kuzalisha upya, kusambaza, au katika njia nyingine yoyote kurudufisha Programu, nzima au kiasi; (e) uza, pangisha, toa leseni, leseni ndogo, sambaza, wajibisha, hamisha au vinginevyo toa haki zozote katika Programu au Huduma, kikamilifu au kiasi; (f) rekebisha, tafsiri, au unda kazi husiani za Programu au Huduma; (g) kupangua, kutokusanya, kugeuza mhandisi au vinginevyo kujaribu kupata, kujenga upya, kutambua au kugundua msimbo wowote wa chanzo, hoja zisizoshughulikiwa, au alogarithimu, au Programu au Huduma kwa njia zozote; (h) kuondoa ilani, lebo au alama zozote za ummiliki kutoka kwenye Programu; au (i) tumia Programu au Huduma kwa malengo ya ulinganishaji na au uwekaji vigezo dhidi ya bidhaa zinazopatikana na watu wengine.

3. HAKI ZA UMMILIKI.

3.1. PROGRAMU NA HUDUMA. Nuance na watoa leseni wake wanamiliki haki zote, kichwa, na faida kwenye Programu na Huduma pamoja na, lakini isiyoegemea katika, haki rasmi zote, hakimiliki, siri ya biashara, alama ya biashara na haki nyingine za mali miliki zilizo hapa, na vichwa vyote vinavyohusiana na haki kama hizo vitasalia tu katika Nuance na/au watoa leseni wake. Kunakili kusikoidhinishwa kwa Programu au Huduma, au kushindwa kuzingatia vikwazo vilivyo hapo juu, kutasababisha usitishaji otomatiki wa Mkataba na leseni zote zilizotolewa hapo, na itafidia faida zote halali kwa Nuance na vyama vyake tanzu kwa kuvunja mkataba.

3.2. PROGRAMU YA MHUSIKA MWINGINE. Huenda programu ikawa na programu ya mhusika mwingine inayohitaji ilani na/au sheria na masharti ya ziada. Ilani kama hizo zinazohitajika za programu ya mhusika mwingine na/au sheria na masharti ya ziada zinapatikana katika http://swype.com/attributions na zinafanywa kuwa mojawapo ya na kushirikishwa na rejeleo kwenye Mkataba huu. Kwa kukubali Mkataba huu, Pia Unakubali sheria na masharti ya ziada, iwapo yapo, na yameelezewa humo.

3.3. DATA YA MATAMSHI NA DATA YA UTOAJI LESENI.

(a) DATA YA MATAMSHI. Kama mojawapo ya Huduma, Nuance hukusanya na kutumia data ya Matamshi, kama ilivyofafanuliwa hapa chini, kusawazisha, kuboresha na kuimarisha utambuzi wa matamshi na vijenzi vingine vya Huduma, na huduma na bidhaa zingine za Nuance. Katika kukubali sheria na masharti ya Mkataba huu, unathibitisha, kuidhinisha na kukubali kuwa Nuance inaweza kukusanya Data ya Matamshi kama mojawapo ya Huduma na kuwa maelezo kama hayo yatatumiwa tu na Nuance au wahusika wengine wanaowajibika chini ya mwongozo wa Nuance, kwa mujibu wa mikataba ya usiri, ili kusawazisha, kuboresha na kuimarisha utambuzi wa matamshi na vijenzi vingine vya Huduma, na bidhaa na huduma nyingine za Nuance. Nuance haitatumia vipengeee vya maelezo katika Data yoyote ya Matamshi kwa lengo lolote isipokuwa kama ilivyoelezwa humo. "Data ya Matamshi" inamaanisha faili za sauti, zinazohusiana unukuzi na faili za kumbukumbu zilizotolewa na wewe humo au kuzalishwa kulingana na Huduma. Data yoyote au yote ya Matamshi unayoitoa itasalia kuwa ya siri na inaweza kufichuliwa na Nuance, iwapo inahitajika, ili kufikia mahitaji ya kisheria ua udhibiti, kama vile chini ya agizo la mahakama au katika taasisi ya serikali iwapo inahitajika au imeidhinishwa kisheria, au katika tukio la kuuza, kuunganisha au kumiliki kwa mhusika mwingine na Nuance.

(b) DATA YA UTOAJI LESENI. Kama mojawapo ya Programu na Huduma, Nuance na wasambazaji wake pia hukusanya na kutumia Data ya Utoaji leseni, kama ilivyofafanuliwa hapa chini. Unathibitisha, ridhaa na kukubali kuwa Nuance inaweza kukusanya Data ya Utoaji Leseni kama mojawapo ya vipengele vya Programu na Huduma. Data ya Utoaji Leseni inatumiwa kusaidia Nuance na wahusika wengine wanaofanya kazi chini ya mwongozo wa Nuance, kwa mujibu wa mikataba ya siri, kuendeleza, kujenga na kuimarisha bidhaa na huduma zake. Data ya Utoaji Leseni inazingatiwa kuwa maelezo yasiyo ya kibinafsi, kwa kuwa Data ya Utoaji Leseni iko katika aina ambayo hairuhusu ushirikiano wa moja kwa moja na mtu yeyete bainifu. "Data ya Utoaji Leseni" inamaanisha ni maelezo kuhusu Programu na kifaa Chako, kwa mfano: chapa ya kifaa, nambari ya muundo, uonyeshaji, ID ya kifaa, anwani ya IP, na data kama hiyo.

(c) Unaelewa kuwa kupitia utumiaji wako wa Programu na Huduma unaiidhinisha ukusanyaji na matumizi kama ilivyoelezewa humo ya Data ya Matamshi na Data Utoaji Leseni, pamoja na uhamishaji katika Marekani na/au nchi nyingine kwa pamoja kwa hifadhi, uchakataji na kutumiwa na Nuance na washiriki wengine.

(d) Data ya Matamshi na Data ya Utoaji Leseni zinazingatia sera ya faragha inayotumika kwa Nuance. Kwa maelezo zaidi angalia sera ya faragha ya Nuance katika http://www.nuance.com/company/company-overview/company-policies/privacy-policies/index.htm.

4. MSAADA. Ili kuharakisha mchakato wa kutathmini na kujaribu Programu na Huduma, Mwenye leseni anaweza kurejelea katika maswali yanayoulizwa sana ya Nuance katika http://www.nuancemobilelife.com. Kwa msaada zaidi, Mwenye leseni anaweza kuomba msaada kama huo kupitia tovuti ya mbele, na baada ya kupatikana kwa mfanyakazi wa Nuance, Nuance inaweza kutoa huduma zinazofaa za msaada kupitia faksi, barua pepe au njia nyingine kwa Mwenye leseni kwa kuzingatia uharibifu na'au ufafanuzi wa utendaji na vipengele vya Programu na Huduma. Msaada wa Nuance utayajibu maswali yako baada ya saa 48 za kazi (bila kujumuisha wikendi na likizo za kisheria / kampuni).

5. KANUSHO LA DHAMANA. UNATHIBITISHA NA KUKUBALI KUWA NUANCE NA WATOA LESENI WAKE NA WASAMBAZAJI WANATOA PROGRAMU NA HUDUMA KWA KO PEKE ILI KUKURUHUSU KWA NA KUTUMIA PROGRAMU NA LESENI. KWA HIVYO, UNAKUBALI KUCHUKUA TAHADHARI NA USALAMAWOTE MUHIMU ILI KULINDA DATA NA MIFUMO YAKO KUTOKANA NA KUPOTEA AU KUHARIBIKA. NUANCE, WATOA LESENI WAKE NA WASAMBAZAJI WANATOA PROGRAMU NA HUDUMA "KAMA ILIVYO," NA MAKOSA YOTE NA BILA DHAMANA YA AINA YOYOTE. KWA MUDA WA JUU ZAIDI ULIORUHUSIWA NA SHERIA ZINAZOTUMIKA, NUANCE, WATOA LESENI WAKE NA WASAMBAZAJI HUSUSAN HUDAI DHAMANA ZOZOTE ZA MOJA KWA MOJA AU ZINAZOTEKELEZWA, PAMOJA NA DHAMANA ZOZOTE ZA WAUZAJI, UBORA KWA LENGO FULANI, AU KUTOKIUKA.

6. KIKOMO CHA DHIMA. KWA KIWANGO CHA JUU KILICHORUHUSIWA NA SHERIA ZINAZOTUMIKA, HAKUNA KATIKA TUKIO LOLOTE AMBAPO NUANCE, MAAFISA, WAKURUGENZI, NA WAAJIRIWA, AU WATOA JI WAKE WA LESENI, WATAWAJIBIKA KWA UHARIBUFU WOWOTE WA MOJA KWA MOJA, KIAJALI, KIMAKSUDI AU MFANO, PAMOJA NA LAKINI BILA KUEGEMEA KATIKA, UHARIBIFU WA KUPOTEZA FAIDA, KUPOTEZA DATA, KUPOTEZA MATUMIZI, UCHACHAWIZAJI WA BIASHARA, AU GHARAMA YA UTUNZI, UNAOTOKANA NA PROGRAMU AU HUDUMA, HATA HIVYO KWA KUSABABISHWA NA , CHINI YA NADHARIA YOYOTE YA MATUMIZI, HATA IWAPO UMESHAURIWA AU MAHALI INGEFAHAMU UWEZEKANO WA UHARIBIFU KAMA HUO MBELENI.

7. KIPINDI NA USITISHAJI. Mkataba unaanza baada ya kukubali Kwako sheria na masharti ya Mkataba na hukwisha muda baada ya usitishaji. Nuance inaweza kusitisha Mkataba huu, na/au leseni zilizotolewa humo, kwa wakati wowote katika uamuzi wake wa pekee, na au bila sababu, kwa kukuarifu kuwa Huduma imekwisha muda au imesitishwa. Mkataba huu utakwisha kiotomatiki baada ya Wewe kuvunja sheria na masharti yoyote. Baada ya kusitisha, utakoma mara moja kutumia na itafuta nakala zote za Programu.

8. UPATANIFU WA UHAMISHAJI. Unawakilisha na kuhakikisha kuwa (i) Huko katika nchi inayozingatia embargo ya Serikali ya Marekani, au aliyotangazwa na Serikali ya Marekani kuwa nchi "inayounga mkono ugaidi"; na (ii) Hujaorodheshwa kwenye orodha yoyote ya Serikali ya Marekani au vyama vilivyo pigwa marufuku.

9. ALAMA ZA BIASHARA. Alama nyingine za biashara, majina ya biashara, majina ya bidhaa na nembo ("Alama za biashara") zilizomo au zinazotumiwa na Programu au Huduma ni alama za biashara au alama za biashara zilizosajiliwa za wamiliki husika, na matumizi ya Alama kama hizo za biashara zitatoa hakikisho la faida kwa mmiliki wa alama ya biashara. Matumizi ya Alama kama hizo za biashara yanakusudiwa zitaashiria ubadilishaji na hazijumuishi: (i) chama tanzu na Nuance na kampuni kama hiyo, au (ii) uidhinishaji au upitishaji wa kampuni kama hiyo ya Nuance na bidhaa au huduma zake.

10. SHERIA INAYOONGOZA. Mkataba huu utaongozwa kwa sheria za Jumuiya ya Madola ya Massachusetts, Marekani, bila kuzingatia migogoro yake ya kanuni za sheria, na unawasilisha katika mamlaka ya kipekee ya mahakama ya shirikisho au jimbo katika Jumuiya ya Madola iliyotajwa kulingana na mzozo wowote unaotokana na Mkataba huu. Mkata huu hautaongozwa na Maafikiano ya Umoja wa Mataifa ya Mikataba kwa mauzo ya Bidhaa Kimataifa, programu ambayo inatengwa moja kwa moja.

11. SHERIA INAYOTOKANA NA MABADILIKO. Unathibitisha na kukubali kuwa Nuance inaweza kubadilisha sheria na masharrti ya Mkatabaa huu mara kwa mara baada ya ilani inayofaa katika anwani uliyotoa baada ya kujisajili, pamoja na anwani yako ya barua pepe. Kama hukubali mabadiliko kama hayo katika Mkataba huu, faida yako tu ni kusitisha kufikia Programu na Huduma. Kuendelea kwako kutumia sehemu yoyote ya Programu au Huduma baada ya kupewa ilani inayofaa na Nuance kuhusu mabadiliko kama hayo kwa ukaguzi wako kutazingatiwa kuwa ukubalifu wako wa mabadiliko kama hayo.

12. SHERIA NA MASHARTI YA JUMLA. Huwezi kuwajibisha au vinginevyo kuhamisha haki au majukumu yoyote chini ya Mkataba huu bila kuzingatia ridhaa ya maandishi ya Nuance. Mkataba huu ni mkataba mzima baina ya Nuance na wewe, na unazidi mawasiliano yoyote mengine au kutangaza kwa kuheshimu Programu. Katika kipengele chochote cha Mkataba huu kinachochukuliwa kuwa batili au kutotekelezwa, vipengele kama hivyo vitakuwa tu kulingana na umuhimu wa kutibu ubatili au kutotekelezwa, na kumbusho la Mkataba huu litaendelea kutekelezwa kikamilifu na mara moja. Kushindwa kwa Nuance kutekeleza au kulazimisha haki yoyote au kipengele cha Mkataba huu hakutajumuisha msamaha wa haki au kipengele hicho. Sehemu 2, 3, 5, 6, 7, 9, 10 na 12 za Mkataba huu zitaendelea kutumika baada ya kwisha muda au kusitishwa kwa Mkataba huu.